Tottenham Hotspurs wamejinasia huduma ya mshambuliaji wa Benfica ya ligi kuu Ureno, Carlos Vinicius kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Vinicius ambaye ni raia wa Brazil ameondoka Benfica akiwa amewafungia jumla ya mabao 24 msimu ulioisha wa ligi kuu Ureno 2019/2020.
Kocha mkuu wa Spurs,Jose Mourinho ana matumaini makubwa kwa Vanicius japo itawalazimu kuweka bilioni 5.7 ili kurasimisha uhamisho wa mshambuliaji huyo hadi kambini mwao kwa mkataba wa kudumu mwishoni mwa msimu huu.