Mshambuliaji mpya wa Yanga Sc,Waziri Junior amechaguliwa kuwa mchezaji bora mwezi Julai wa ligi kuu ya Vodacom (VPL), msimu wa 2019/20 ndani ya klabu yake aliyokuwa akiitumikia hapo awali ya Mbao Fc.
Wazir alitupia jumla ya mabao matano kwenye mechi tano za mwezi Julai ambayo yaliipa nafasi timu yake kujitoa kwenye nafasi ya 19 mpaka kufika nafasi ya 16 ikiwa na pointi 45.