Home Makala Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Taifa Stars

Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Taifa Stars

by Sports Leo
0 comments

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa anategemewa leo kuwa mgeni rasmi wa mechi ya kirafiki iliyopo kwenye ratiba ya FIFA baina ya Taifa Stars ya Tanzania na timu ya Taifa ya Burundi.

Dk Hassan Abbasi ambaye ni katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amethibitisha kuwepo kwa Majaliwa kama mgeni rasmi kwenye mchezo huo unaoongozwa na nahodha Mbwana Samatta.

Mechi hiyo inayohusisha wachezaji wa Stars wanaocheza ndani na nje iliweka kambi Oktoba 5 na kuanza kufanya mazoezi rasmi Oktoba 6 ambapo ni mchezaji mmoja aliondolewa kwenye ile orodha ya kwanza ambayo ilijumisha wachezaji 25.

banner

Nyota huyo ni John Bocco wa Simba ambaye anasumbuliwa na majeraha aliyoyapata kwenye klabu yake ya Simba.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited