Site icon Sports Leo

Winga Simba Atua Polisi Tanzania

Polisi Tanzania inazidi kukisuka upya kikosi chake tayari kwa msimu ujao wa ligi kuu bara ambapo hivi leo wameidaka saini ya mchezaji wa Simba Sc ,Rashidi Juma kwa kandarasi ya mwaka mmoja.

Juma ametua Polisi Tanzania kwa mkopo baada ya kuona mabosi wake wa Simba Sc wakisaili namba nyingi zenye ushindani na kujikuta yeye akiishia benchi.

Wachezaji wengine waliotambulishwa hadi sasa Polisi Tanzania ni Daruweshi Saliboko wa Lipuli Fc,Kassim Shabani Haruni (Sahare All Stars),Datus Peter(Mbao Fc) na Ramadhani Kapera wa KMC.

Exit mobile version