Pamoja na kuibuka na ushindi dhidi ya klabu ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu siku ya Jumapili bado takwimu zinaonyesha kuwa klabu ya Yanga sc msimu huu haishkiki baada ya kufanya mambo makubwa kadhaa katika msimamo wa ligi kuu nchini mpaka kufika raundi ya 12.
1.Kukaa Kileleni mwa Msimamo
klabu hiyo chini ya udhamini wa Gsm msimu huu imekaa kileleni mwa ligi kuu tangu ianze ikiwa mpaka sasa imefikia katika raundi ya 12 ambapo imecheza jumla ya michezo 12 ikishinda michezo kumi na kutoa sare katika michezo miwili dhidi ya Simba sc na Namungo Fc kitu ambacho kinawafanya wakae kileleni mwa msimamo na alama 32.
2.Idadi ya Magoli ya kufunga
Mpaka sasa klabu ya Yanga sc ndio timu yenye idadi kubwa ya magoli ya kufunga ikiwa imefunga jumla ya magoli 22 katika mechi 12 huku ikiwa imeruhusu nyavu zao kuguswa mara nne tu ikiwa na wastani wa 18 ukijumlisha magoli yote ya kushinda na kufungwa ikizifunika timu zote za ligi kuu hata zikiungana na kujumlisha wastani wao wa magoli bado Yanga sc itakua ipo juu.
3.Soka la Kuvutia
Klabu Yanga sc inapokua na mastaa wote wa kikosi cha kwanza wakiwemo Yanick Bangala na Khalid Aucho wamekua na mpira unaovutia hasa wakimilika eneo katikati mwa uwanja huku usumbufu wa mshambuliaji Fiston Kalala Mayele ukiwa na mwiba kwa mabeki wa timu pinzani kiasi cha kufanikiwa kuchukua alama katika viwanja vigumu kama vile Mkwakwani Tanga yalipo makao ya Coastal Union sehemu ambayo ni ngumu kwa Yanga sc kuchukua alama tatu hasa miaka ya hivi karibuni.