Klabu ya Yanga sc ipo tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Tanzania Prisons utakaofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya jioni ya saa 10.
Tayari kikosi kamili cha klabu hiyo kipo jijini humo kwa ajili ya mchezo huo na leo kocha Miloud Hamdi amethibitisha utayari wa kikosi chake wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini humo.
“Maandalizi yetu yapo vizuri sana, tuna fainali nne za kucheza. Tupo tayari kuukabili mchezo wa kesho kikamilifu. Kila mchezaji anajua kitu gani cha kufanya kesho. Kikosi chetu kipo kamili hakuna majeruhi wapya. Hatuna presha yoyote na hatuna sababu ya kuwa na presha”alisema kocha huyo.
Mchezo huo wa ligi kuu ya NBC kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Yanga SC utachezeshwa na mwamuzi Abdallah Mwinyimkuu kutoka mkoani Singida, atasaidiwa na Makame Mdogo wa Shinyanga na Wema Kalinga wa Dodoma Dodoma.