Site icon Sports Leo

Yanga Sc Kugomea Fainali Crdb

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe kwenye mkutano wake na waandishi wa Habari uliofanyika  Juni 9, 2025 katika makao makuu ya klabu hiyo amesema kuwa klabu hiyo haitacheza fainali ya Kombe la CRDB hadi pale watakapolipwa fedha za ubingwa wa Kombe hilo kwa msimu uliopita.

Kamwe alisisitiza kuwa tangu mwaka jana wamekua wakiandika barua kwa katibu mkuu wa Shirikisho la soka nchini Wilfred Kidao kuomba fedha hizo bila mafanikio.

“Taarifa hii iwafikie ofisi ya Katibu mkuu wa TFF na Wadhamini wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB, kuwa HATUTACHEZA mchezo wa Fainali wa CRDB siku ya tarehe 28, mpaka tutakapolipwa hela yetu ya Ubingwa kwa msimu uliopita. Tumevumilia dharau hizi kutoka kwa Mamlaka za Soka kwa muda mrefu sana, sasa imefika mwisho. Hii ya Zanzibar pia HATUCHEZI”.Alisema Kamwe kwa hisia kali

“Tumeshaandika sana barua tunazungushwa tu, Sasa nimesikia wanatangaza kuwa fainali itachezwa Zanzibar tuwaambie kuwa hata hiyo fainali hatuchezi mpaka tulipwe fedha zetu za ubingwa uliopita,” amesema Kamwe.

Yanga sc waliibuka mabingwa wa kombe la shirikisho la Crdb baada ya kuifunga timu ya Azam Fc kwa penati 6-5 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Amaani Complex uliopo visiwani Zanzibar.

 

Exit mobile version