Sports Leo

Yanga Sc Njia Nyeupe kwa Gilbertinho

Klabu ya Petro de Luanda imepanga kusitisha mkataba wa winga , Deivi Gilberto, aliyejiunga na klabu hiyo kwa mkopo kutoka Orlando Pirates kutokana na mchezaji huyo kuwa utovu wa nidhamu klabuni hapo na kushindwa kuitumikia Petro de Luanda kwa usahihi.

Taarifa zinaripoti kuwa winga huyo amekuwa na tabia mbaya nje ya uwanja jambo ambalo Klabu hiyo imechoshwa na tabia hiyo. Aidha awali kulikuwa na taarifa za chini Kuwa klabu kutoka Tanzania zinahitaji saini yake lakini bado hakuna klabu iliyoweka wazi kama inahitaji saini ya winga huyo.

Yanga sc ni miongoni mwa klabu ambayo ilikuwa inatajwa kuhitaji saini ya winga huyo , mpaka wakati hii tayari Yanga wameshamalizana na Mshambuliaji wao Musonda ambae hatakuwa sehemu ya Kikosi hicho msimu ujao hivyo taarifa zinaripoti kuwa nafasi yake atachukua winga huyo.

Exit mobile version