Sports Leo

Yanga sc Vs Kmc Machi 19

Bodi ya ligi kuu Tanzania bara imetangaza kusogeza mbele kwa baadhi ya michezo ya ligi kuu nchini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uwanja wa Mkapa kuwa na matumizi mengine ya kiserikali.

Katika Taarifa yake kwa vyombo vya habari nchini bodi hiyo imesogeza mbele mchezo kati ya klabu ya Yanga sc dhidi ya Kmc kutoka machi 16 hadi machi 19 kutokana na sababu ya uwanja wa Benjamini Mkapa kuwa na matumizi mengine hivyo mchezo kusogezwa kwa siku tatu mbele.

Yanga sc itavaana na Kmc ikiwa na kumbukumbu ya kushinda kwa jumla ya mabao 2-0 katika mchezo wa awali uliofanyika katika uwanja wa majimaji mkoani Songea kwa mabao ya Fiston Mayele na Feisal Salum.

Exit mobile version