Ilikua raha kama kulamba asali ya nyuki wadogo,Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mashabiki na viongozi wa klabu ya Yanga sc kutoka na furaha uwanjani kufuatia ushindi wa klabu hiyo dhidi ya Tabora United katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani humo.
Mchezo huo ambao ulitanguliwa na tambo nyingi nje ya uwanja kufuatia kuwapo kwa maneno mengi baina ya mkuu wa mkoa huo Mh.Paul Chacha pamoja na Msemaji wa Tabora United Christina Mwagala dhidi ya Ally Kamwe mkuu wa idara ya habari ya Yanga sc.
Yanga sc ikiwakosa Khalid Aucho na Stephan Aziz Ki ambao ni majeruhi huku Cletous Chama na Kennedy Musonda wakikosekana kutokana na kuchelewa kujiunga na timu hiyo kutoka timu ya Taifa ya Zambia.
Yanga sc ilianza kupata bao la kwanza kwa faulo kali iliyopigwa na Israel Mwenda dakika ya 57 ya mchezo huo baada ya Dube kuangushwa karibu na eneo la hatari.
Mapumziko timu hizo zilikwenda Yanga sc akiongoza kwa bao hilo japo Tabora United walijitahidi kutoa upinzani mkali.
Kipindi cha pili Yanga sc waliendelea kushambulia kwa kasi kupitia kwa Clement Mzize na Dube huku akiiingia Jonathan Ikangalombo akichukua nafasi ya Maxi Nzengeli aliyeumia.
Mzize alifunga bao la tatu kwa Yanga sc dakika ya 57 ya mchezo akimchungulia kipa wa Tabora United baada ya kupokea pasi nzuri ya Pacome Zouzoua na dakika ya 68 Dube alifunga bao la tatu kwa Yanga sc akimalizia pasi ya Pacome Zouzoua ndani ya eneo la hatari.
Tabora United inabidi washukuru washambuliaji wa Yanga sc ambao walikosa baadhi ya nafasi za kufunga magoli kwa maana ingekua aibu kubwa kama wangefungwa mabao matano kama ilivyowatokea wapinzani wengine.
Yanga sc sasa imefikisha alama 61 katika michezo 23 ya ligi kuu ya Nbc nchini ikiwa kileleni mwa msimamo huku Tabora United wakiwa nafasi ya tano ya msimamo na alama 37 wakicheza michezo 24 ya ligi kuu ya Nbc nchini.