UONGOZI wa klabu ya Yanga pamoja na kikosi chao leo Jumapili asubuhi wamekua miongonj mwa wananchi waliofika katika msafara wa kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Yanga jana Jumamosi jioni ilisimamisha kambi yao na kutoa fursa kwa wachezaji wao leo Jumapili kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa Rais huyo aliyeaga Dunia Machi 17 jioni baada ya kuugua ugonjwa wa moyo.
Wachezaji na viongozi wa klabu hiyo walikutana makao makuu ya klabu saa 3:00 asubuhi kisha ndio msafara wao ukaanza kwenda katika uwanja wa Uhuru.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kupitia katika ukurasa wao rasmi wa Instagram ulielezea kuwepo kwa tukio hilo kwa wachezaji na viongozi wao siku ya leo.
Shughuli za kuaga mwili wa marehemu Magufuli zilianza jana kwa kuongozwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mawaziri, viongozi na kufuatiwa na wananchi wa kawaida.