Mabao mawili ya Aziz Ki na Kennedy Musonda yameiwezesha klabu ya Yanga sc kuibuka na alama tatu katika mchezo wa awali wa michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Asas Fc ya Djibout.
Mchezo uliofanyika katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es salaam ambapo Yanga sc ilikua mgeni ilifanikiwa kutawala dakika zote tisini za mchezo japo ufanisi mdogo katika safu ya ushambuliaji uliwafanya kumaliza mchezo ikiwa na mabao hayo mawili pekee.
Safu ya ushambuliaji chini ya Kennedy Musonda na Clement Mzize mpaka sasa bado inashindwa kumalizia nafasi nyingi wanazopata Yanga sc licha ya kupewa mipira lukuki na safu ya kiungo ya klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika Augusti 26 ambapo Yanga sc itakua mwenyeji na utafanyika katika uwanja huo huo ambapo mshindi wa jumla michezo hiyo miwili atafuzu hatua ya pili ambapo watakutana na mshindi kati ya Al-Merreck na Otoho d’oyo.