Site icon Sports Leo

Yanga sc Yapangwa na Wadjibout Cafcc

Klabu ya Yanga itaanza hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Asas FC ya Djibouti ikianzia ugenini na kumalizia Uwanja wa Mkapa, Dar na mshindi atacheza wa mechi ya AS Otoho ya Congo na Al Merrikh ya Sudan.

Yanga sc ikifanikiwa kupata matokeo katika michezo hiyo minne,miwili ya raundi ya awali na miwili ya hatua ya pili basi moja kwa moja itakua imefuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika na endapo ikitolewa basi haina budi kusubiri msimu ujao kwani kwa sasa hakuna ule utaratibu wa kuangua kombe la shirikisho endapo utatolewa hatua ya pili kama awali.

Asas FC msimu uliopita walimaliza nafasi ya pili kati ya timu kumi na sita zilizoshiriki ligi kuu ya soka nchini humo hivyo ni timu ambayo inafungika kwa kuangalia rekodi za Yanga sc za hatua ya kimataifa kwa msimu uliopita huku wakiwa na faida ya kuanzia ugenini na katika hatua ya pili itabidi wakaze buti kupambana na vigogo wa Al Merreckh Fc ambao wanapewa nafasi kubwa ya kupita dhidi ya As Otoho ya Congo.

Yanga sc wanahukumiwa zaidi ya matokeo yao ya msimu uliopita ambapo walifika fainali ya kombe la shirikisho licha ya kukosa kombe lililochukuliwa na Usm Algers hivyo msimu huu mashabiki na wadau wa soka wana matarajio makubwa kwa kikosi hicho.

 

Exit mobile version