Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kurejea katika kilele cha ligi kuu nchini baada ya kuibuka na alama tatu katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons Fc katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam majira ya saa moja usiku.
Ikiingia uwanjani bila kocha mkuu wake Nasreddine Nabi ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu ya ligi kuu pamoja na mshambuliaji kiongozi Fiston Mayele mwenye majeraha timu hiyo ilishindwa kuifungua safu ya ulinzi ya klabu ya Prisons ambao waliamua kupaki basi muda mwingi wa mchezo huo.
Licha ya kufanya mabadiliko mara kadhaa ikiwaingiza Farid Musa,Djuma Shabani na Benard Morrison Yanga sc ililazimika kusubiri mpaka dakika ya 89 ya mchezo ambapo Feisal Salum aligongeana vizuri na Farid Musa na kuandika bao pekee katika mchezo huo ambalo lilibeba matumaini ya mashabiki wengi wa klabu hiyo ambao bado wanasherehekea kucheza michezo 49 ya ligi kuu bila kupoteza.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc sasa imefikisha alama 35 za ligi kuu ikicheza michezo 14 na kukaa kileleni huku Simba sc ikiwa nafasi ya pili na alama 34 katika michezo 15 na Azam Fc ipo nafasi ya tatu na alama 32 ikicheza michezo 14.