Sports Leo

Yanga Sc Yawabakisha Duke,Nzegeli

Klabu ya Yanga sc imetangaza kuwa mastaa wawili wa klabu hiyo Duke Abuya na Maxi Nzengeli wamesaini mikataba mipya ya miaka miwili kuendelea kusalia klabuni hapo baada ya mikataba yao kutamatika msimu huu.

Mabosi wa klabu hiyo wameridhishwa na michango ya mastaa hao klabuni hapo na kuamua kuwatunuku mikataba hiyo ili kuendelea kuhudumu katika eneo la klabu hiyo.

Yanga Sc Yawabakisha Duke,Nzegeli-sportsleo.co.tz

Duke ambaye alijiunga na Yanga sc akitokea Singida Black Stars kwa mkataba wa mwaka mmoja ikiwa ni pendekezo la kocha Miguel Gamondi huku pia Nzengeli akisajiliwa kama mchezaji asiye na jina kutoka As Maniema Union ya Congo Dr.

Kinyume na matarajio ya wengi wachezaji hao wameibuka kuwa tegemeo kikosini humo wakionyesha viwango bora zaidi na kuwavutia makocha wote watatu waliofundisha klabu hiyo msimu uliopita.

Miguel Gamondi aliwapa nafasi mara nyingi ya kuanza na hata alipokua Sead Ramovic naye aliwatumia katika eneo la kiungo na mwisho kocha Miloud Hamdi naye aliwapa nafasi mpaka katika michezo migumu dhidi ya Simba Sc na Singida Black Stars.

Exit mobile version