Timu ya wananchi Yanga leo imemshusha Bongo Carraca Antonio Domingoz Pinto ambaye alikuwa mtendaji Mkuu wa klabu ya Ureno Benfica kwa miaka 10 ili kuanza kazi ya kushauri kueleka mabadiliko ya kimfumo ya uendeshaji wa klabu.
Nguli huyo wa mfumo wa soka la kisasa ameletwa kwa hisani kubwa ya kampuni ya Gsm ambao ni wadhamini wakubwa wa Yanga sc.
Carraca Antonio amepokelewa leo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM Mhandisi Hersi Said.