Klabu ya Yanga kupitia kwa mdhamini wao kampuni ya GSM jana Januari 30,20 wamefanikisha kutoa masaada wa fedha na mahitaji ya chakula cha miezi mitatu pamoja na gharama ya matibabu ya Anna Majaliwa.
Yanga imetoa msaada huo kwenye familia ya Anna ambaye anasumbuliwa na tatizo la mwili kukosa fahamu ndani ya miaka mitatu jambo lililompelekea kushindwa kupata choo kwa zaidi ya miezi sita.
Akizungumza Anna alisema kuwa alipata tatizo hilo kwa zaidi ya miaka hiyo mitatu jambo linalomfanya kupata tabu kila kukicha hivyo anawashukuru sana Yanga kupitia mdhamini wao GSM kwa kutambua tatizo lake.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.