Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ametoa muda wa wiki moja kwa uongozi wa Yanga kumlipa stahiki zake,Zahera aliyerejea nchini wiki iliyopita ametishia kwenda kushitaki FIFA kama hatakamilishiwa malipo yake
Mkongomani huyo kwa sasa yuko nchini kwa takribani wiki ya pili ambapo ametishia kuwa atapeleka malalamiko FIFA na Yanga italazimika kumlipa hata gharama anazotumia sasa wakati akisubiri kulipwa stahiki zake.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amemtaka Zahera kuwa na subira kwani atalipwa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.