Home Makala Zahera Aipa Ushindi Simba sc

Zahera Aipa Ushindi Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Kuelekea mchezo wa klabu bingwa hatua ya makundi kati ya Simba sc dhidi ya As Vita Club kocha wa zamani wa klabu ya Yanga sc Mwinyi Zahera ameipa asilimia kubwa klabu ya Simba kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Zahera anayefahamika nchini kwa kupenda kusema ukweli katika soka amesema kuwa klabu ya As vita ya msimu uliopita ni tofauti na ilivyo sasa baada ya kuondokewa na mastaa wengi wakiwemo kina Mkoko Tonombe na Tuisila Kisinda huku Jean Makusu na wengineo huku Simba sc ikiwa imeboreka katika baadhi ya maeneo.

“As Vita iliyoifunga Simba bao 5-0 imesambaratika Kwakuwa wachezaji takribani 10 waliokuwepo kikosini wameondoka wakiwemo Fabrice Ngoma, Jean Makusu, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda na wengine bora.

banner

“Kwasasa nimewafuatilia As Vita katika mechi 5 za ligi, bado wana vijana wengi hawana experience na champions league huku Simba msimu huu imebalance, Washambuliaji, Kiungo na beki zimeimarika, na wanawachezaji wazoefu”.

“Naipa Simba Asilimia 60 kushinda, wakati AS Vita naipa asilimia 40” alimalizia kocha huyo wakati akiongea na Redio ya East Afrika katika Kipyenga.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited