Home Makala Zahera Apewa Bosi Mpya Drc

Zahera Apewa Bosi Mpya Drc

by Sports Leo
0 comments

Shirikisho la soka la Kongo limemteua kocha Christian Nsengi Bembe  kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Kongo akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Jean Florent Ibenge Ikwange aliyejiuzulu siku chache zilizopita kutokana na matokea yasiyoridhisha katika michuano ya Afcon nchini Misri.

Nsengi alikuwa Mkurugenzi wa benchi la ufundi la klabu hiyo na kocha wa timu ya taifa hilo ya U23 ambapo atasaidiwa na Christopher Oualembo na Mwinyi Zahera. Kocha wa makipa atakuwa mlinda mlango wa zamani wa Tp mazembe Robert Kidiaba huku Kocha wa washambuliaji atakuwa Treasure Lualua.

Meneja wa timu atakuwa Dodo Landu na katibu wa timu atakuwa Azizi Makukula ambapo wote kwa pamoja watakua na kazi ya kurejesha makali ya kikosi hicho kuelekea hatua za awali za mashindano ya kufuzu kombe la dunia.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited