Home Masumbwi Kiduku amtaka aliyempiga Dulla Mbabe

Kiduku amtaka aliyempiga Dulla Mbabe

by Dennis Msotwa
0 comments

Bondia Twaha Kiduku ameonesha nia ya kuhitaji pambano baina yake na bondia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Tshimanga Katompa ambaye alimpiga bondia mwingine wa Tanzania Abdallah Pazi maarufu kama Dulla mbabe siku ya Jumamosi katika pambano lililopewa jina la Kiboko ya Wageni.

Katika kuonesha kutofurahishwa kupigwa na kudhalilishwa kwa Dulla Mbabe,Twaha amewaomba mapromota wa ngumi nchini kuandaa pambano hilo mapema ili yeye aweze kurudisha heshima ya nchi.

banner

Twaha Kiduku hajapigana tangu ampige Dulla mwezi Agosti mwaka huu na amesema kuwa atajiandaa vya kutosha kuhakikisha anashinda endapo pambano hilo likiwepo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited