Home Masumbwi Mwakinyo Ambwaga Indongo

Mwakinyo Ambwaga Indongo

by Dennis Msotwa
0 comments

Bondia Hassan Mwakinyo amefanikiwa kutetea ubingwa wake wa African Boxer Union(ABU) baada ya kufanikiwa kumpiga bondia kutoka nchini Namibia Julius Indongo katika raundi ya nne kwa Knoukout baada ya kumpiga ngumi mfululizo hadi mwamuzi alipoingilia kati.

Katika pambano hilo lililopewa jina la ‘mabingwa wa ulingo’lilifanyika katika ukumbi wa hotel ya Ubungo plaza ambapo kuanzia raundi ya kwanza Mwakinyo alionyesha nia yake ya kutetea mkanda baada ya kurusha ngumi kwa mipango huku akijihami zaidi.

Umri mkubwa ulionekana kuwa kikwazo kwa Indongo baada ya kukosa stamina mara kwa mara huku alipofika raundi ya nne alizidiwa na makonde mfululizo hali iliyomlazimu mwamuzi kumaliza pambano ili kumuokoa bondia huyo.

banner

Katika mahojiano baada ya mchezo bondia Mwakinyo alisema ushindi wake ni kudra za mwenyezi mungu huku Indongo akisema hajui amepigwaje pigwaje huku akitupia lawama kwa mwamuzi kuwa aliwahi kumaliza pambano.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited