Bondia Mtanzania ambaye pia ni bingwa wa Afrika Hassan Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni usiku wa leo katika pambano la kimataifa la kutetea mkanda wa Africa Boxing Union (ABU) kwa uzito wa light middleweight dhidi ya Mmalawi Julius Indongo.
Pambano hilo litafanyika hapa nchini katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam ambalo litakuwa ni la raundi 12 na litarushwa hewani na kituo cha azam media.
Indongo anayeishi Marekani mpaka sasa amekwishapigana mapambano 23 proffesional akipoteza mapambano matatu tu huku akishinda 12 kwa knockout,pia amewahi kuwa bingwa wa WBO upande wa Afrika.
Katika hatua nyingine bondia mwingine kutoka Tanzania Tony Rashid naye atapambana ulingoni kutetea ubingwa wa African Boxing Union Super Bantam title dhidi ya Bongani Mahlangu wa Afrika Kusini katika pambano la raundi 12.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mapambano mengine ya utangulizi yanatarajiwa kuanza mida ya saa kumi na mbili jioni.