Mwanariadha Alphonce Felix Simbu kutoka Tanzania ametwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya marathon ya wanaume, katika mbio za Championship za Dunia (World Athletics Championships) zilizofanyika Tokyo, Japani.
Ushindi huo ni wa kihistoria kwa sababu ni mara ya kwanza kwa Tanzania kushinda medali ya dhahabu katika mbio hizo maarufu za Dunia au mashindano ya Olimpiki katika riadha kama yanavyotamkwa mara nyingi.
Simu na Amanal Petros wa Ujerumani walimaliza kwa muda ule ule – saa 2:09:48 lakini Simbu aliweza kumshinda Petros kwa muda wa sekunde 0.03, kutokana na mwendo wa haraka wa mbio za kumalizia mashindano hayo (photo finish) katika mbio hizo zilizomaziwa ndani ya uwanja wa kitaifa wa Japan.
Mwanariadha Iliass Aouani wa Italia alishinda medali ya fedha baada ya kushika nafasi ya pili na kutwaa medali ya tatu katika historia yake ya mashindano hayo ambapo alitumia muda wa 2:09:53.
Mbio zilikuwa zenye ushindani mkubwa, zikiwa zimeanza kwa nafasi kubwa ya washiriki katika kundi kuu, lakini kadri kilomita zilivyokwisha, baadhi ya wanariadha walianguka nyuma kutokana na hali ya joto na uchovu huku Wanariadha kutoka Ethiopia waliotarajiwa kama wenye nguvu hawakuweza kudumu hadi mwisho akiwemo miongoni mwao, Tadese Takele na Deresa Geleta walipungua kasi kabla ya kumaliziwa kwa mbio.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hii ni mara ya kwanza kwa Simbu kutwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya dunia, baada ya kushinda medali ya shaba mwaka 2017 katika World Championships. Pia alipata nafasi ya pili (runner-up) katika mbio za Boston Marathon mwaka huu nchini Marekani.
Simba alisema kwamba alijiamini, lakini hakujua kama angeweza kushinda mpaka wanateknojia walipoonyesha kwamba lipo jina lake juu katika matokeo ambapo ushindi wake umetawala vichwa vya habari nchini Tanzania na Asia Mashariki kwa ujumla, kwani amelipa heshima kubwa nchi yake katika michezo ya kimataifa.
Tayari Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan amempongeza mwanariadha huyo kupitia mitandao yake ya kijamii kutokana na kuipa heshima nchi ya Tanzania kwa kutwa medali hiyo.