Home Riadha Kilimarathon Kufanyika Feb 25,2025

Kilimarathon Kufanyika Feb 25,2025

by Sports Leo
0 comments

Mashindano ya riadha ya Kilimanjaro Marathon yanatarijiwa kufanyika mwakani tarehe 15 Februari mkoani Kilimanjaro baada ya kufanyiwa uzinduzi rasmi katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Usajili wa washiriki wa mbio hizo unatarajiwa kufunguliwa rasmi Disemba mosi mwaka huu ambapo washiriki watashindana katika mbio za 42.2 km (Kili Premium Lager Full Marathon),21.1km (Tigo Kili Half Marathon) pamoja na 5km.

Katika ufunguzi huo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, Stephen Mpeka alishiriki kukata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa mbio za Kilimanjaro Premium Lager international Marathon 2024 katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam ambapo pia alisindikizwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group, Jose Moran, Katibu Mkuu Chama Cha Riadha Tanzania, Jackson Ndaweka, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael na Afisa Maendeleo ya Michezo wa Baraza la Michezo Tanzania, Charles Maguzu.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited