Inadaiwa kwamba klabu ya Yanga sc na Mbeya city Fc zimekubaliana kuuziana mchezaji Kibu Dennis kwa gharama zinazokadiriwa kufikia shilingi milioni 150 kwa mkataba wa miaka minne.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya kuwa na mazungumzo kwa muda mfupi huku dau hilo likijumuisha na kununua mkataba wake uliobaki katika klabu ya Mbeya city ambapo timu hizo zimekubaliana.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani hivi sasa imebaki mchezaji kusaini mkataba pekee ambapo atajiunga nan Yanga sc mwishoni mwa msimu huu.