Adam Adam wa JKT Tanzania ni miongoni mwa mastraika wazawa wenye mabao mengi Ligi Kuu Bara msimu hii (mabao saba).
Mshambuliaji huyo hataki kuongelea ishu ya kwenda kufanya majaribio nchini Uturuki, ingawa anakiri kuwa ni kweli alikwenda na kwamba mwenye mamlaka ya kulizungumzia hilo ni wakala wake anayeishi nje.
“Ninachojua April kila kitu kitakuwa wazi, ila siwezi kuzungumza ni kwa namna gani, lakini pia nilijifunza mengi sana Uturuki kwa muda wa wiki mbili nilizokaa huko, kama kujitambua na kuishi maisha sahihi ya soka, mtazamo wangu kuwa mpana kuliko kushindwa na vitu dhaifu,” anasema.