Baada ya kushindwa kutinga hatua ya mtoano kufuzu michuano ya kombe la dunia nchini Qatar 2022,Afrika Kusini wanajipanga kutuma malalamiko rasmi kwa shirikisho la soka duniani(FIFA) juu ya maamuzi ya penati ya utata yaliyowapa nafasi Ghana ya kusonga mbele.
Katika mchezo huo wa mwisho wa kundi uliofanyika Accra Ghana,Afrika Kusini walikua wanahitaji alama moja tu huku wenyeji wakihitaji zote tatu kusonga mbela huku Ghana akiibuka na ushindi wa 1-0 kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Andrew Ayew.
Penati hiyo ilitokea dakika ya 33 baada ya mpira wa kona uliongia ndani ya kumi na nane na mwamuzi kudai kuwa umeshikwa na mchezaji wa wageni na kuamuru kupigwa kwa adhabu hiyo.
Mtendaji mkuu wa chama cha soka Afrika Kusini (SAFA) Tebogo amesema kuwa wamepanga kuviandika barua CAF na FIFA kuchunguza mchezo uliovoendeshwa na bbadhi ya maamuzi yaliyochukuliwa.
”Tayari tulimwambia match commissioner kwamba tutaadika malalamiko yetu.
Kama FIFA watajiridhisha na malalamiko hayo wanawezo kuamuru mchezo huo kama ilivyofanya mwaka 2018 katika mchezo wa kufuzu michuano hiyo kati ya Afrika Kusini na Senegal.