Nyota mpya wa Kano Pillars ya Nigeria Ahmed Musa (28) amegoma kusafiri na klabu kwenda mikoani bila usafiri wa ndege akidai kusafiri kwa basi umbali mrefu sio salama kwake. Nyota huyo wa zamani wa Leicester City atacheza mechi za nyumbani tu.
Musa aliyewika katika ligi kuu nchini Uingereza alijiunga na timu hiyo kama mchezaji huru lakini ametoa masharti ya kucheza mechi za nyumbani tu katika uwanja wa Sani Abacha huku pia atacheza zile za karibu ikiwa watamhakikishia usalama wake huku akihitaji usafiri wa ndege kwa mechi za mbali.
Staa huyo kutokana na masharti hayo atakosa michezo dhidi ya Warri Wolves na Plateau United kutokana na kutokuwapo kwa usafiri wa ndege huku uongozi wa klabu hiyo ukikubalina na wazo la nyota huyo ambaye aliitumikia timu hiyo wakati anaanza soka kati ya 2009 mpaka 2012.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.