45
Klabu ya Zamalek ya Misri imeongea na Wakala wa Kiungo Mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe,Khama Billiant juu ya kumsajili Kiungo huyo wa Kaizer Chiefs ambapo maslahi Binafsi yameshaafikiwa huku akiwa amebakiza mkataba wa miezi sita tu na Kaizer Chiefs.
Zamalek wanataka kumsajili Billiant kwa dau la Dola milioni 1.5 ambazo Ni zaidi ya shilingi bilioni tatu za Kitanzania na mshahara wake atakuwa analipwa Dola Laki nane (800,000) ambazo Ni zaidi ya shilingi bilioni 1.7 za Kitanzania.
Billiant mwenye umri wa Miaka 30 Mpaka sasa ameshacheza jumla ya michezo 311 akifunga Magoli 85 na assist 84.
Cc:Viwanjanileo