Mshambuliaji wa Mbeya City Fc Eliud Ambokile amejiunga na wababe wa soka la Afrika kutoka Kongo Tp Mazembe kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Black Leopard ya Afrika ya Kusini alipokua anacheza kwa mkopo.
Inadaiwa klabu hiyo ambayo ni mabingwa mara tano wa klabu bingwa Afrika wamelipa takribani shilingi milioni 50 ili kupata saini ya mshambuliaji huyo mfupi mwenye nguvu na kasi anayetumia vizuri mguu wa kulia.
Ambokile amesajiliwa na Tp Mazembe ili kuziba nafasi ya mshambualiaji Ibrahim Ajibu ambaye walitaka kumsajili lakini walishindwana maslahi binafsi na mchezaji huyo huku taarifa zikidia tayari mchezaji huyo alikua na mkataba na Simba sc.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Inatarajiwa Ambokile ataanza kuonekana na Mazembe katika michuano ya kombe la Kagame yatakayofanyika Kigali nchini Rwanda ambapo Mazembe watakua wageni waalikwa.