Site icon Sports Leo

Ame Afungiwa,Simba sc Yapigwa Faini

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemfungia Mchezaji wa Klabu ya Simba SC, Ibrahim Ame Mohamed michezo mitatu (3) na faini ya Tsh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kumzuia Mwamuzi msaidizi wa mchezo kufanya kazi yake.

Tukio hilo lilitokea katika mchezo kati ya Simba Sc na Gwambina FC uliochezwa Aprili 24, 2021 kwenye uwanja wa Gwambina mkoani Mwanza.

Mwamuzi huyo, Godfrey Msakila ameondolewa katika ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitatu (3) kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo huo.

Katika Mechi hiyo hiyo, Simba SC imetozwa faini ya Tsh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la Mashabiki wake kurusha chupa tupu na zenye maji uwanjani na kusababisha mpira kusimama kwa zaidi ya dakika hadi Polisi kuingilia kati kutuliza ghasia hiyo.

Exit mobile version