Staa wa zamani wa Manchester united Anderson Oliveira amestaafu kucheza soka la ushindani akiwa katika klabu ya Adama Demirspor inayoshiriki ligi daraja la pili nchini uturuki.
Staa huyo mshindi wa kiatu cha dhahabu mwaka 2007 alihamia manchester united akitokea Fc Porto ya Ureno ambako alionyesha uwezo mkubwa akitokea Gremio ya kwao nchini Brazil.
Licha ya kuaminiwa mara kadhaa na kocha Alex Ferguson Anderson alishindwa kuwa na ubora unaofanana kwa muda mrefu huku majeruhi yakichangia hali iliyosababisha kuachana na united mwaka 2015 na kujiunga na As Roma ambako hakudumu na kurudi nchini kwao katika klabu ya Internacional.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Licha ya kuitumikia timu hiyo katika michezo 11 msimu uliopita staa huyo atabakia klabuni hapo akipewa kazi katika klabu hiyo baada ya kukubali kupunguziwa mshahara wake na ataangwa rasmi tarehe 12 october.