Kikosi cha Simba sc kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kina mechi zake nne kwa mwezi Aprili kusaka pointi tatu muhimu katika Ligi Kuu Bara.
Kwenye msimamo kiksoi hicho kipo nafasi ya pili na pointi zake ni 46 baada ya kucheza mechi 20 huku ikibakiwa na viporo viwili.
Ratiba yake ambayo imetolewa leo Machi 31 itaanza Aprili 14 ambapo itakua ni Simba v Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mkapa huku wakiwa na kumbukumbu ya hapo awali kutoa sare katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. huku ratiba nyingine ikiwa ni:
Mwadui FC v Simba itakuwa Aprili 18, Uwanja wa Kambarage.
Kagera Sugar v Simba itakuwa ni Aprili 21, Uwanja wa Kaitaba.
Gwambina v Simba ni Aprili 24, Uwanja wa Gwambina Complex.
Simba v Dodoma Jiji itakuwa ni Aprili 27, Uwanja wa Mkapa.