Home Soka Arsenal gari limewaka,yatinga nusu fainali carabao

Arsenal gari limewaka,yatinga nusu fainali carabao

by Dennis Msotwa
0 comments

Kinda wa Arsenal Eddie Nketia ameiongoza Arsenal kufuzu nusu fainali ya kombe la ligi maarufu kama carabao cup baada ya kuwachakaza Sunderland kwa kipigo kikubwa cha 5-1 usiku wa kuamkia leo kwenye dimba la Emirates Jijini London.

Eddie alifungua mvua hiyo ya mabao dakika 17 akimalizia kazi ya kichwa ya beki Bob Holding,aliongeza goli la pili dakika ya 49 kabla ya kukamilisha hat trick yake dakika 58 akimalizia pasi nzuri kutoka kwa Nicolas Pepe.

Magoli mengine ya Arsenal yalifungwa na Pepe dakika ya 27 pamoja na kinda Patino aliyecheza mechi yake ya kwanza ya wakubwa,ushindi huo umemfurahisha kocha mkuu wa timu hiyo Mikel Arteta aliyekuwa akitimiza miaka miwili ya kibarua chake ndani ya klabu hiyo.

banner

Arteta alifanya mabadiliko tisa kwenye kikosi kilichanza mchezo huo toka kile kilichopata ushindi wa 4-1 dhidi ya Leeds united kwenye ligi kuu soka nchini Uingereza.

Ushindi huo ni wan ne mfululizo kwa timu hiyo ndani ya mwezi Disemba wakiwa katika kiwango bora kabisa,washika bunduki hao sasa wanasubiria mechi za leo ili kujua ni timu ipi watakayocheza nayo kwenye hatua ya fainali.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited