Home Soka Arsenal kuendeleza ushindi dhidi ya Spurs?

Arsenal kuendeleza ushindi dhidi ya Spurs?

by Sports Leo
0 comments

Washika bunduki wa London Arsenal watashuka dimbani jioni ya leo katika mchezo wa ligi kuu soka ya Uingereza dhidi ya wapinzani wao wa jadi Tottenham Hotspurs katika dimba la Emirates.

Baada ya kuanza vibaya ligi hiyo kwa kupoteza michezo mitatu ya mwanzo Arsenal wameshinda mechi zao tatu za mwisho mbili za ligi kuu na moja ya kombe la ligi tena bila kuruhusu bao lolote hali inayowapa kujiamini zaidi.

Totenham wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita kwa mabao 3-0 nyumbani dhidi ya Chelsea.

banner

Matokeo mengine ya ligi hiyo jana yameshuhudia Chelsea na Man Utd wakipoteza alama tatu muhimu kwenye mbio za ubingwa huku Liverpool wakilazimishwa sare na Brentford.

Chelsea walipoteza kwa 1-0 dhidi ya Man City,Man Utd wakishangazwa na Villa Old Trafford kwa 1-0 na Liverpool wakishikwa shati kwa sare ya 3-3 na Brentford katika mchezo wa kusisimua.

Arsenal wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kikosi kamili bila majeruhi,mchezo mwingine ya ligi hiyo leo;

Southampton vs Wolvehampton (saa 10:00 jioni)

 

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited