Klabu ya soka ya Arsenal imeshindwa kupata ushindi katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu soka nchini Uingereza baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Brentford iliyopanda daraja msimu huu.
Brentford ilijipatia uongozi kunako dakika ya 22 kupitia kwa Sergi Canos,kabla ya kuongeza lingine dakika ya 73 kupitia Christian Norgaard na kuzima ndoto za Gunners kuondoka na pointi katika mchezo huo.
Arsenal ilimkosa nahodha wake Pierre Aubameyang pamoja na straika Alexander Lacazete waliopata majeraha madogo kuelekea mchezo huo uliopigwa katika dimba la Brentford Community Stadium Magharibi mwa London.