Home Soka Arsenal yaivimbia Liverpool Carabao

Arsenal yaivimbia Liverpool Carabao

by Sports Leo
0 comments

Licha ya kucheza pungufu kwa takribani dakika 60 za mchezo wa nusu fainali ya kombe la carabao washika bunduki wamefanikiwa kutoa sare ya bila kufungana dhidi ya Liverpool.

Mchezo huo wa raundi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la ligi umefanyika katika dimba la Anfield Jijini Liverpool.

Kiungo wa kati wa Arsenal Granit Xhaka ameendeleza wimbi la kukusanya kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi hiyo kwa kumpiga teke la tumbo mshambuliaji wa Liverpool Diogo Jota dakika ya 30 ya mchezo na kuwaacha wenzake wakiwa pungufu kwa kipindi kirefu.

banner

Baada ya kadi hiyo kocha wa Arsenal Mikel Arteta aliamua kubadili mfumo kutoka 4-2-3-1 na kuhamia 3-5-1 ambao uliweza kuwadhibiti vilivyo majogoo wa Anfield na kumaliza mchezo huo bila ya kupiga shuti lolote langoni.

Mchezo wa marudiano utafanyika wiki ijayo katika dimba la Emirates Jijini London kutafuta timu itakayoifuata Chelsea kwenye fainali ya kombe hilo itakayofanyika mwezi February katika dimba la Wembley.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited