Klabu ya Arsenal imefikia makubaliano na klabu ya Brighton and Hove Albion kumsajili beki wa kati Muingereza Ben White kwa ada ya paundi milioni 50.
Ben aliitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya England kwenye michuano ya Euro 2020.
Beki huyo alicheza kwa kiwango kikubwa akiwa kwa mkopo Leeds United na kuisaidia kupanda daraja msimu wa 2020/2021 hali iliyopelekea klabu yake mama ya Brighton kumrudisha na kumpa mkataba wa miaka minne.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Brighton ilikataa ofa mbili za Arsenal kutokana na Ben kuzivutia timu nyingine kubwa kama Everton na Man Utd, Mchezaji huyo kwasasa yup mapumzikoni hivyo atafanyiwa na kutambulishwa atakaporudi.