Beki Benjamini Asukile wa Prisons amekumbana na adhabu ya kufungiwa mechi tano pamoja na faini ya kiasi cha shilingi laki tano kufuatia kutoa shutuma za rushwa kwa klabu ya Yanga sc katika mchezo wa raundi ya nne ya kombe la shirikisho la Azam.
Baada ya mchezo huo uliomalizika kwa Yanga sc kuondoka na ushindi wa bao moja lililofungwa na Yacouba Sogne,Asukile alifanya mahojiano na Televisheni ya Azam na hapo akatoa shutuma hizo ambazo hazikua na uthibitisho tofgauti na maelekezo ya kanuni za mashindano hayo.
Katika barua ya kumfungia iliyotolewa na Tff imesema kwamba adhabu hiyo ataitumika kwa mechi zote za mashinano rasmi yaliyochinin ya shirikisho hilo.