Kiungo wa kimataifa wa Uganda Khalid Aucho amejiunga na klabu ya soka ya Yanga akitokea klabu ya soka ya Misr Lel Makkasa ya Misri kwa mkataba wa miaka miwili.
Kiungo huyo alikua pia akihusishwa na kujiunga na wekundu wa Msimbazi lakini ni Wananchi ndio walioshinda vita hiyo ya mafahali wawili wa soka la Tanzania.
Aucho amesema kuwa mazungumzo mazuri kati yake na Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM Injinia Hersi ndiyo yaliyomshawishi kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.