Licha ya kumtimua Kocha Arstica Cioaba klabu ya Azam Fc bado imeendelea na wimbi la kuwa na matokeo mabovu katika michezo ya ligi kuu nchini baada ya leo kulazimishwa sare ya 1-1 na Biashara United katika uwanja wa Karume mkoani Mara.
Ayoub Lyanga aliipa Azam Fc uongozi dakika ya 20 lakini bao hilo lilisawazishwa na Thomas Omwenga dakika ya 58 kwa shuti kali na kumshinda kipa David Mapigano.
Biashara inabidi wajilaumu wenye baada ya kukosa penati baada ya mchezaji wao kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la mita 18 lakini mpigaji alikosa penati hiyo baada ya kupiga nje.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.