Home Soka Azam Fc Wamtangaza Msemaji Mpya

Azam Fc Wamtangaza Msemaji Mpya

by Sports Leo
0 comments

 

Taarifa kutoka klabu ya Azam Fc kuhusu uteuzi wa nafasi ya mkuu wa kitengo cha habari ya mawasiliano inasomeka kama ifuatavyo.

UONGOZI wa Azam FC unayofuraha kumtangaza mwandishi mkongwe, Thabith Zakaria ‘Zaka Za Kazi’, kuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano.

banner

Zakaria anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaffar Idd, aliyepangiwa majukumu mengine ndani ya kampuni.

Ujio wa Zakaria ni sehemu ya jitihada za uongozi wa Azam FC kuboresha kitengo cha habari ndani ya timu, ambapo sasa kitatambulika kama Kitengo cha Habari na Mawasiliano kitakachokuwa kikiongozwa naye.

Tunaamini ya kuwa Zakaria atatumia vilivyo uzoefu mkubwa aliokuwa nao katika tasnia ya habari, alioupata wakati akifanya kazi na makampuni makubwa ya habari ya IPP Media na Azam TV, na kuitangaza vema timu yetu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited