Klabu ya soka ya Azam Fc imekamilisha usajili wa golikipa wa KMKM ya Zanzibar Ahmed Suleiman ‘Salula’ kwa mkataba wa miaka miwili kukipiga katika viunga vya Chamazi.
Golikipa huyo anaenda kuchukua nafasi ya mlinda mlango David Kisu ambaye amefunguliwa mlango wa kutokea kuelekea Namungo Fc.
Azam Fc inaonekana kujidhatiti katika kuelekea msimu ujao wakidhamiria kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali kwa kufanya usajili wa nguvu na wa mapema.