Site icon Sports Leo

Azam fc,Namungo Hakuna Mbabe

Mechi kati ya Azam Fc na Namungo Fc imemalizika kwa sare baada ya dakika 90 za mchezo uliofanyika katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaaam.

Mabao ya Azam Fc yalifungwa na Idd Nado dakika za 19 na 74 huku Namungo wakifunga kupitia kwa Charles Manyama dakika ya 25 huku Stephen Sey akifunga bao la kusawazisha dakika za mwisho mwa mchezo.

Sare hiyo inamaanisha kwamba Azam Fc imeshindwa kupata ushindi katika mechi tano mfululizo na kuzidi kuacha pengo la alama kwa Yanga sc wenye alama 34 huku Azam Fc wakiwa na alama 27.

Exit mobile version