Home Soka Azam,Wazimbabwe Hapatoshi Chamazi

Azam,Wazimbabwe Hapatoshi Chamazi

by Dennis Msotwa
0 comments

Ni ngumu kutabiri lakini ndio hivyo patakua hapatoshi katika uwanja wa chamazi siku ya jumapili ambapo kutachezwa mchezo wa kimataifa kuwania kufuzu hatua ya makundi kombe la shirikisho kati ya Azam fc na Triangle United.

Mchezo huo utakaopigwa siku ya jumapili majira ya saa kumi jioni utakuwa ni mchezo wa awamu ya kwanza huku ule wa marudiano ukifanyika baada ya wiki mbili nchini Zimbabwe.

Azam imepata ahueni baada ya kurejea kwa kiungo Mudathir Yahaya japo ana nafasi finyu ya kutumika katika mechi ya jumapili kutokana na kukosa utimamu wa mwili lakini uwepo wa Idd Seleman,Frank Domayo na Abubakar Salum utachagiza ushindi kwa wanalambalamba hao.

banner

Katika kuhakikisha wanapata sapoti ya kutosha Azam fc wameweka viingilio vya shilingi 3000 kwa mzunguko na elfu 5000 kwa daraja la kati huku V.i.p ikiwa ni shilingi elfu 10000.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited