Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mbeya City Fc sasa klabu ya Simba sc inahitaji alama tatu tu ili kutwaa taji la ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya nne mfululizo.
Endapo klabu hiyo itafikisha alama hizo itakua imetwaa taji hilo baada ya kujihakikishia kwamba hakuna timu ambayo itazifikia alama hizo huku ikiwa tayari Azam Fc waliokatika nafasi ya tatu wakiwa wamekosa uwezekano wa kuwa mabingwa baada ya Simba sc kufikisha alama 73 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yeyote isipokua Yanga sc.
Mchezo unaofata wa ligi kuu utakua baina ya timu hizo zilizopo nafasi ya juu ya msimamo na endapo Yanga sc watafungwa basi Simba sc watatawazwa mabingwa kupitia mchezo huo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.