Home Soka Balama Nje Wiki Tano

Balama Nje Wiki Tano

by Dennis Msotwa
0 comments

Licha ya kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi sita sasa mchezaji Balama Mapinduzi ataendelea kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tano nyingine baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika ya kusini.

Balama alirejea nchini jana na kupokelewa na Afisa Habari wa klabu ya Yanga sc Hassan Bumbuli ambaye alithibitisha kuwa baada ya oparesheni hiyo kuonyesha mafanikio sasa mchezaji huyo atakua nje ya uwanja kwa wiki tano zaidi kabla ya kuanza mazoezi mepesi mepesi.

Balama anakumbukwa na mashabiki wa soka nchini baada ya kumtungua kipa Aishi Manula kwa shuti la mbali katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara ulioisha kwa sare ya 2-2 mwanzoni mwa mwaka jana.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited