Klabu ya Barcelona imemfuta kazi kocha Enesto Vervede baada ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha licha ya kuongoza msimamo wa ligi kuu nchini humo(La liga).
Vervede alijiunga na Barca mwaka 2017akitokea Athletic Bilbao na amefanikiwa kuipa timu hiyo ubingwa wa ligi kuu mara mbili.
Licha uongozi wa timu hiyo kufanya mazungumzo na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Xavi Hernandez ili kumrithi Vervede, timu hiyo imemteua Quique Satien kuwa kocha mkuu akitokea Real Betis.