Klabu ya Bayern Munich imefanikiwa kuifikia rekodi ya Fc Barcelona ya kuvuna makombe sita kwa msimu mmoja baada ya jana kufanikiwa kuifunga timu ya Tigres katika mchezo wa fainali ya klabu bingwa duniani katika mchezo uliofanyika nchini Qatar.
Bao pekee la Benjamin Pavard liliihakikishia Bayern taji la sita ndani ya miezi sita huku mastaa mbalimbali wa timu hiyo wakitwaa tuzo binafsi.
Kutwaa kwa taji hilo kumeifanya timu hiyo kuifikia rekodi iliyowekwa na Barcelona mwaka 2009 huku pia likiwa ni taji la sita kwa kocha wa klabu hiyo Hans Flick tangu aanze kuifundisha timu hiyo mwezi novemba 2019.